17 Februari 2016 - 16:44
Ujerumani yasisitiza pendekezo la eneo lisiloruka ndege Syria

Makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za magharibi na ghuba yamejikuta yakikimbia na kuacha silaha baada ya majeshi ya Syria yakisaidiwa na Urusi na Iran kushadidisha mashambulizi dhidi ya magaidi hao ili kuokoa miji iliyotekwa na magaidi hao na hatimaye kuruhusu wananchi kurudi kwenye makazi yao.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa:  Katika kuonyesha kutetea upande wa magaidi nchini Syria Kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel leo  amerudia katika  hotuba  aliyoitoa  bungeni  leo pendekezo lake la kuwa  na  eneo  ambalo  haliruhusiwi  ndege  kuruka nchini  Syria ambako  raia  watalindwa, wazo  ambalo limepuuziwa  haraka  na  Urusi , ambayo  imesema  hatua hiyo  inawezekana  tu  kwa  ridhaa  ya  serikali  ya  Syria.

Ujerumani na washirika wake wa Ulaya , Marekani na waarabu wanataka kutumia njia hiyo kuwapa nafasi magaidi kama walivyofanya nchini Libya na kupelekea utawala wa Gaddafi kuanguka na kusababisha hali ya amani kupotea kabisa nchini humo mpaka hivi sasa.

Mjini  Damascus , zaidi  ya  malori 100 yaliyobeba  mahitaji ya  kiutu  yalitarajiwa  kuondoka  kwenda  katika  maeneo matano  yanayokaliwa na magaidi yaliyozingirwa  na  majeshi  nchini  humo, ikiwa  ni sehemu  ya  juhudi zinazoelezwa  na  afisa  mmoja  wa Urusi  kuwa  ni  hatua  ya  kwanza  kuelekea  utekelezwaji wa  makubaliano  yaliyofikiwa  miongoni  mwa  mataifa yenye  nguvu duniani  mjini  Munich  wiki  iliyopita.

Mjumbe  wa  Umoja  wa  Mataifa  Staffan de Mistura amekuwa  akijaribu  kuhakikisha kwamba   misaada  hiyo inaimarisha nafasi  ya  kuanza  tena  mazungumzo  ya amani  kabla ya  kufikia  mwisho  wa  mwezi  huu.

Lakini  juhudi  hizo zimetiwa  kiwingu  na  mapigano  makali kaskazini  mwa  Aleppo, ambako  makundi  mbali  mbali yanayoungwa  mkono  na  mahasimu  wa  kikanda  na kimataifa  wanakabiliana  kukamata  sehemu  ya eneo  la ardhi  linalounganisha  mji  wa  pili  kwa  ukubwa  nchini Syria na  mpaka  na  Uturuki.

Makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za magharibi na ghuba yamejikuta yakikimbia na kuacha silaha baada ya majeshi ya Syria yakisaidiwa na Urusi na Iran kushadidisha mashambulizi dhidi ya magaidi hao ili kuokoa miji iliyotekwa na magaidi hao na hatimaye kuruhusu wananchi kurudi kwenye makazi yao.

Mwisho wa habari/ 291